Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi RSF hajajibu ombi la kuzidisha muda wa kusitisha mapigano

Kiongozi RSF Hajajibu Ombi La Kuzidisha Muda Wa Kusitisha Mapigano Kiongozi RSF hajajibu ombi la kuzidisha muda wa kusitisha mapigano

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa kundi la la Rapid Support Forces la Sudan ambalo linapigana na jeshi la nchi hiyo hajaitikia wito wa kuongezwa kwa muda wa usitishaji mapigano uliopo.

Kusitishwa kwa mapigano kumetatizwa na mapigano na milio ya mizinga katika baadhi ya maeneo ya Sudan. Waziri wa mambo ya nje wa nchi jirani ya Sudan Kusini ambaye anaongoza juhudi za upatanishi ameambia BBC kuwa anatumai Jenerali Hamdan Dagalo atakubali ombi hilo. Jeshi la Sudan linasema kiongozi wake ametoa kibali chake cha awali kwa ombi hilo na kutuma mwakilishi kwa mazungumzo ya ana kwa ana.

Usitishaji vita wa sasa nchini Sudan umejaribiwa vikali na mapigano yanayoendelea karibu na mji mkuu na maeneo mengine ya nchi. Lakini bado inaruhusiwa kwa watu wa Khartoum kupata bidhaa zinazohitajika kama chakula na maji pamoja na kuwahamisha raia wa kigeni.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza amesema iwapo makubaliano hayo, ambayo yataisha baada ya saa chache, hayatarefushwa - juhudi za London kuwaokoa raia wa Uingereza hazitawezekana.

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan awali amekubali kurefusha muda wa usitishaji mapigano hadi Jumapili na kutuma mwakilishi katika nchi jirani ya Sudan Kusini kwa mazungumzo, lakini mpinzani wake Jenerali Hamdan Dagalo bado hajajibu.

Majirani wa Sudan ambao wanajaribu kumaliza mzozo huo wanatumai hatua hiyo itakuwa msingi wa mwanzo wa mazungumzo ya ana kwa ana ambayo yanaweza kumaliza mzozo huo.

Chanzo: Bbc