Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi Gabon akataa mshahara wa Urais

Marekani Yasitisha Msaada Kwa Gabon Kufuatia Mapinduzi Kiongozi Gabon akataa mshahara wa Urais

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema amesema hatapokea mshahara wake kama Rais na badala yake atapokea mshahara wake kama kamanda wa kijeshi.

Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya kijeshi, Nguema ambaye ni rais wa mpito aliyeingia madarakani baada ya kupinduliwa kwa Rais Ali Bongo mwezi Agosti, amechukua hatua hiyo kutokana na mahitaji mengi ya watu wa Gabon.

Mbali na kutopokea mshahara wa urais, Jenerali Nguema pia ameamua kupunguza matumizi ya fedha za umma kwa kupunguza posho kwa wabunge, kuondoa fedha za kisiasa na kupunguza marupurupu ya vikao kwa lengo la kuimarisha hazina ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live