Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi Chad awasamehe walioandamana kumpinga

Chad Kiongoziii Kiongozi Chad awasamehe walioandamana kumpinga

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jenerali Mahamat Idriss Derby kiongozi wa Chad ametoa msamaha kwa watu wengine 110 waliohukumiwa jela kwa kushiriki maandamano ya fujo dhidi ya serikali ya nchi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana.

Maandamano ya kupinga kuongezwa muda wa kipindi cha utawala wa mpito wa Deby yalifanyika huko N'Djamena mji mkuu wa Chad na katika miji mingine ya nchi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana.

Jeshi la Chad lilimtangaza Deby kuwa mkuu wa nchi na jeshi mnamo Aprili 2021 baada ya kifo cha baba yake, Idriss Deby Itno, ambaye aliuawa wakati wa operesheni dhidi ya waasi baada ya kusalia madarakani nchini humo kwa miaka 30.

Dikrii iliyosainiwa na kiongozi wa Chad inaeleza kuwa: "Watu waliofunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kwa makosa ya kufanya mikutano na maandamano kinyume cha sheria, kufanya hujuma za makusudi, kuharibu mali n,k kufuatia matukio ya Oktoba 20 wananufaika na msamaha wa Rais. Maandamano ya Oktoba 2022

Vijana wa kiume zaidi ya 600 wakiwemo watoto wasiopungua 80 walitiwa mbaroni huko N'Djamena mji mkuu wa Chad Oktoba 20 mwaka jana na katika siku kadhaa zilizofuatia; na kisha walipelekewa gerezani katika mji unaopatikana jangwani wa Koro Toro umbali wa zaidi ya kilomita 600 kutoka N'Djamena.

Watu hao walihukumiwa bila ya uwakilishi wowote wa kisheria baada ya kushikiliwa kwa miezi kadhaa.

Katika kipindi cha chini ya miezi minne mamlaka husika za Chad zimewasamehe watu 436 waliopatwa na hatia ya kushiriki katika maandamano ya fujo ya Oktoba mwaka jana. Watu hao waliokuwa wakipinga kurefushwa muhula wa mpito wa kiongozi wa Chad wamesamehewa na mamlaka husika za nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live