Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kioja baada ya chatu mkubwa kutembelea kaburi la mshika nyoka kumuomboleza

22fe788b2eac194f Kioja baada ya chatu mkubwa kutembelea kaburi la mshika nyoka kumuomboleza

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Chatu huyo alijoteza siku mbili baada ya William Ewoi kuzikwa nyumbani kwake Inaaminka kujitokeza kwa mnyama huyo ni ishara ya heshima kwa mshikaji wakeMwanawe William, Vincent Ewoi, alikaribisa tukio hilo akisema kuwa ni ishara marehemu baba yao ambaye aliwaenzi nyoka, ameenda nyumbani

Wakazi wa kijiji cha Kampi Samaki katika kaunti ya Baringo walipigwa na butwaa baada ya chatu mkubwa kuingia nyumbani kwa mshikaji wake ambaye alizikwa Alhamisi, Julai 8.

Chatu huyo alijiteza siku mbili baada ya William Ewoi kuzikwa nyumbani kwake akijitembeza kwenye kaburi lake kana kwamba anatoa heshima zake za mwisho.

Mnyama huyo alikuwa anajishughulisha na vya kwake pasi kusumbuliwa na kelele za wanakijiji ambao walikuwa wamefika nyumbani kwa Ewoi kushuhudia maajabu hayo.

Inaaminka kujitokeza kwa chatu huyo ni ishara ya kutoa shukrani na heshima kwa mshikaji wake ambaye alimlinda vyema akiwa bado hai.

Read also

Mzee wa Legio Maria Aliyetabiri Ajali ya Homabay Miongoni Mwa Wahanga

Akizungumzia kisa hicho, mwanawe mzee huyo mwenye umri wa miaka 86, alisema kilikuwa ishara ya bahati nzuri.

Vincent Ewoi, alikaribisha tukio hilo akisema kuwa ni ishara marehemu baba yao ambaye aliwaenzi nyoka, ameenda nyumbani

Vincent alisema kabla ya kifo cha baba yake, alikuwa amesema nyoka watarejea nyumbani.

Si mchawiVincent pia alipuzilia mbali dhana kwamba baba yake alikuwa mchawi kwa sababu ya kushika nyoka.

Badala yake alisema baba yake alikuwa anawashika wanyama hao, anawatoa sumu na kuwachezesha mbele ya watalii ambao walikuwa wakitembelea Ziwa Baringo.

Sumu hiyo ilikuwa inauzwa nchini na mataifa ya kigeni.

“Hii si uchawi kabisaaa kwa sababu kama familia imekuwa ndio njia ya kujipatia mkate.Baba yetu alikuwa akifanya biashara nao na kuwauza, Alitufunza kufuga nyoka na kuwala," alisema Vincent.

Mkewe marehemu Easter Ewoi, alisema hawatamuua chatu huyo akiongezea kuwa wataendelea kuwatibu wanaoumwa na nyoka kama alivyokuwa akifanya William.

William alikuwa ameheshimiwa na Makavazi ya Kitaifa akitajwa kama mshika nyoka mwenye kipaji na talanta.



Read also

Mmoja Akamatwa kwa Kutangaza Kifo cha Rais Yoweri Museveni

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke