Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinyang'anyiro cha urais nchini Liberia chaingia duru ya pili

Kinyang'anyiro Cha Urais Nchini Liberia Chaingia Duru Ya Pili Kinyang'anyiro cha urais nchini Liberia chaingia duru ya pili

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika mwezi ujao nchini Liberia kufuatia kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uchaguzi ambapo Rais George Weah na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai wote hawakupata wingi wa kura kuweza kushinda uchaguzi huo.

Bw Weah alipata 43.83% ya kura huku Bw Boakai, aliyekuwa makamu wa rais akipata 43.44%.

Uchaguzi wa Oktoba 10 ulikuwa wa mchuano mkali zaidi wa urais nchini Liberia tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika takriban miongo miwili iliyopita.

Duru ya pili ilitabiriwa, lakini Bw Boakai, 78, amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa kwa kukaribia hesabu ya Bw Weah.

Ilibidi duru ya pili ya uchaguzi kufanyika kwani hakuna mgombeaji aliyepata zaidi ya 50% ya kura katika duru ya kwanza. Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika tarehe 14 Novemba, mkuu wa tume ya uchaguzi Davidetta Browne alisema baada ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Bw Boakai alimfuata Bw Weah katika duru ya kwanza ya upigaji kura katika uchaguzi wa 2017, na akapoteza ushindi katika kura ya mchujo kwa kura nyingi.

Chanzo: Bbc