Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda mtanzania anaecheza soka Uingereza akumbwa na Corona

100585 Mnoga+pic Kinda mtanzania anaecheza soka Uingereza akumbwa na Corona

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini England katika klabu ya Portsmouth, Haji Mnoga amebainika kuambukizwa virusi vya Covid-19 zinazosababuisha ugonjwa wa corona. Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo na kuthibitishaa na Mnoga mwenyewe zimefichua kuwa, beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 17 ni miongoni mwa wachezaji wanne waliogundulika na maambukizi hayo ndani ya klabu hiyo iliyowahi kutamba kwenye Ligi Kuu ya nchini humo (EPL). "Baada ya kupokea vipimo vya kundi la pili, Portsmouth inathibitisha kwamba Haji Mnoga naye amebainika kuwa na Virusi vya Corona," taarifa hiyo imesomeka hivyo na kuongeza; "Hii inafuatia wachezaji wengine watatu, James Bolton, Andy CannonĀ  na Sean Raggett nao kubainika navyo hivyo wachezaji hao wote wanne wamejitenga binafsi wakifuata maelekezo ya afya ya serikali." Klabu inawatakia afya njema na kwa sasa inasubiria majibu ya vipimo vingine 10 na inaendelea kukumbusha watu wafuate maagizo ya serikali juu ya kujikinga," iliongeza taarifa ya klabu hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mnoga amesema kuwa afya yake inaendelea vyema. "Nashukuru kila mmoja kwa meseji zenu. Mimi na familia yangu tunaendelea vizuri kufuata protokali. Naamini kila mmoja atakaa salama," ameandika Mnoga.

Chanzo: mwananchi.co.tz