Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachoendelea Niger baada ya tishio la Nigeria

Niqer Tishio Nigeria.jpeg Kinachoendelea Niger baada ya tishio la Nigeria

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Majeshi ya Niger jana Jumamosi alitoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kujiweka katika hali ya tahadhari baada ya rais wa Nigeria na jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS kutishia tena kuivamia kijeshi nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, "Moussa Salau Parmo," Mkuu wa Jeshi la Niger, jana (Jumamosi, Agosti 26), alitoa amri kwa vikosi vyote vya ulinzi vya nchi hiyo kuwa kwenye hali ya tahadhari baada ya kutolewa tena vitisho vya kuvamiwa kijeshi Niger.

Taarifa ya mkuu huyo wa jeshi la Niger iliyotangazwa redioni imesema: "Mara baada ya kupokea ujumbe huu, vikosi vyote vya jeshi vinatakiwa kuwa macho na kukaa katika hali ya tahadhari."

Mkuu wa Majeshi ya Niger amesema kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuongezeka vitisho vya kuvamiwa nchi, na madhumuni yake ni kuepuka "kushitukizwa umma" na kushindwa kutoa majibu yanayofaa.

Majenerali wa ECOWAS wametishia tena kuivamia kijeshi Niger

Mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na makamanda wa kikundi cha kijeshi kinachojulikana kwa jina la Baraza la Taifa la Ulinzi wa Nchi" yalitokea nchini Niger tarehe 26 mwezi uliopita wa Julai bila ya kufyatuliwa risasi hata moja. Siku moja baadaye, makamanda wa kijeshi wa baraza hilo walitangaza kupitia televisheni kuwa wamechukua madaraka ya nchi.

Baada ya kutokea mapinduzi hayo, rais aliyeondolewa madarakani amekuwa kizuizini yeye na familia yake katika Ikulu ya Rais. Mipaka yote ya Niger ilifungwa, bunge na serikali ilivunjwa na katiba ilisitishwa kutokana na “hali ya usalama kuzidi kuwa mbaya na na kutokana na mtikisiko wa kijamii na kiuchumi uliotokea baada ya mapinduzi hayo ya kijeshi.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuwa imejiandaa kuingilia kijeshi nchini Niger baada ya kushindwa mazungumzo ya kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Muhammad Bazoum.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live