Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimbunga Khanun chaua 34 Japan

Kimbunga Khanun Chaua 34 Japan Kimbunga Khanun chaua 34 Japan

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Kimbunga kimepiga eneo la Kusini mwa Japan, na kulazimisha maelefu ya watu kuhama na kusababisha umeme kukatika karibu robo tatu ya nyumba zote kwenye visiwa vya Okinawa.

Kimbunga Khanun kinachosonga mbele polepole - ni cha tatu kupiga Asia Mashariki katika wiki kadhaa - kikitishia kuzidisha mvua kubwa zaidi huko Beijing katika kipindi cha zaidi ya karne moja.

Kimbunga hicho kilichosababisha mafuriko pia kimsababisha vifo vya takriban watu 34 nchini China hadi sasa. Wataalamu wanasema kwamba hali mbaya ya hewa kama hii itatokea mara kwa mara kwa sababu ya ongezeko la joto duniani.

Khanun kinakuja baad aya vimbunga vingine viwili, Talim na Doksuri, kusababisha dhoruba kali, ambayo pia iligusa Ufilipino na Taiwan, na kuua zaidi ya watu 30, katika wiki chache zilizopita.

Visiwa vya joto vya Japan vya Okinawa vinatarajiwa kukabiliwa na dhoruba ya kimbunga hocho kasi ya kilomita 252 kwa saa (156mph) siku ya leo Jumatano.

Takriban watu 20,000 wameshauriwa kuhama na takriban safari 900 za ndege zimekatishwa katika uwanja wa ndege wa Naha wa Okinawa. Huu ni msimu wa kilele wa watalii kwa kisiwa hicho. Dhoruba kali kama hizo ni nadra wakati huu wa mwaka huko Japani.

Chanzo: Bbc