Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimbunga Freddy kurudi tena Msumbiji

Shule Zafungwa Huku Kimbunga Kikikaribia Madagascar Kimbunga Freddy kurudi tena Msumbiji

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimbunga Freddy kinatarajiwa kutua pwani ya kusini mwa Afrika Jumamosi, baada ya kusababisha vifo vya takriban watu 27 nchini Msumbiji na Madagascar kilipotua kwa mara ya kwanza mwezi uliopita.

Wanasayansi wanasema mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha vimbunga kuwa na mvua kubwa na upepo mkali zaidi.

Raia nchini Msumbiji wanajitayarisha kwa mvua kubwa wakati kimbunga hicho kikitarajiwa kutua kwa mara ya pili nchi humo tukio ambalo si la kawaida, wataalamu wanasema.

Maelfu ya watu tayari wameachwa bila ya makaazi. Huenda zaidi ya watu nusu milioni wakawa katika hatari ya janga la kibinaadamu mara hii, kwa mujibu wa mashirika ya kupambana na majanga nchini.

Idara ya hali ya hewa duniani (WMO) inasema kimbunga Freddy kinaaminika kuelekea kuwa kimbunga cha muda mrefu. Rekodi ilioko sasa ya muda wa kudumu kimbunga ni siku 31.

Kilianza kutoka pwani ya Australia kaskazini mapema Februari na baadaye kusafiri kuelekea maelfu ya kilomita katika bahari Hindi kutoka mashariki hadi magharibi, na kuviathiri visiwa vya Mauritius na RĂ©union, kabla ya kutua Madagascar wiki mbili baadaye hatimaye kuelekea Msumbiji.

Idara hiyo ya hali ya hewa duniani inasema ni nadra kwa kimbunga kuzunguka na kurudi tena na wamekitaja kama tukio la kushangaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live