Kimbunga Freddy kimeripotiwa kukaribia Mauritius ambapo safari za ndege nchini humo zimesitishwa rasmi.
Taarifa kutoka nhcini humo zinaeleza kuwa, Mauritius pia imefunga soko lake la hisa wakati upande wa pili Madagascar imeandaa timu za dharura kwa ajili ya mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Kimbunga Freddy kina upepo mkali unapenda kwa kasi ya mpaka kilomita 120 kwa saa, ambapo angalizo limetolewa kutokwenda maeneo ya baharini
Video fupi imesambaa ikionesha upepo mkali na mawimbi yakipiga hoteli moja iliyoko ufukweni mwa bahari nchini Mauritius huku maji yakiingia kwenye ukumbi wa hoteli wakati wageni na wafanyakazi wakitazama.