Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimbunga Batsirai kuipiga Madagascar

Kimbungaa Kimbunga Batsirai kuipiga Madagascar

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimbunga Batsirai kinatarajiwa kukipiga kisiwa cha Madagascar leo kwa dhoruba kali ambayo upepo wake utakua ukivuma kwa kasi ya kilometa 235 kwa saa.

Watabiri wa hali ya hewa wamesema dhoruba kamili itawasili kisiwani humo kuanzia jioni hii au baadae usiku, huku wakionya kutakuwa na madhara makubwa hususan mafuriko upande wa mashariki na eneo la kati ya Madagascar.

Kama sehemu ya tahadhari watu 22,000 wamehamishwa na kupelekwa kwenye majumba yanayotumika kwa mazoezi, majengo ya shule na hata makanisani hususan kwenye pwani ya mji wa Mananjary.

Umoja wa Mataifa umesema ndege za uokozi na boti zimewekwa tayari na maandalizi yamefanyika kwa ajili ya usambazaji wa mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live