Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimbuka chasababisha uharibifu Msumbiji

5b28710dc3d1287a7bb852e14953b434 Kimbuka chasababisha uharibifu Msumbiji

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSUMBIJI imekumbwa na mafuriko yaliyotokanana kimbunga Eloise kilichopita katikati ya mji wa Beira upepo ukiwa ni kilomita 160 kwa saa.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Msumbiji (INAM) imeeleza kuwa Beira ilipokea milimita 250 za mvua katika kipindi cha saa 24.

Serikali na Mashirika ya misaada yanachunguza kiwango cha uharibifu ulitokana na Kimbunga hicho ili kuwasaidia waathirika.

Pia serikali ipo inajitahidi kurudisha umeme na mawasiliano ambayo yalikatwa katika baadhi ya maeneo huku baadhi ya watu wakiripotiwa kufariki kutokana na kimbunga hicho.

Kwa mujubi wa Msimamizi wa Taasisi ya Majanga, Antonio Beleza amesema hadi sasa zaidi ya nyumba 1,000 zimeangamizwa na nyingine 3,000 zikiharibika huku zaidi ya watu 160,000 wakiathiriwa.

Chanzo: habarileo.co.tz