Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomkuta aliebeti na hela za Boss

WhatsApp Image 2021 12 10 At 13.jpeg Kilichomkuta aliebeti na hela za Boss

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Kenya, Robert M'munoru mwenye umri wa miaka 20 kutoka Kaunti ya Lamu ametoweka na hajulikani alipo hadi sasa baada ya kutumia pesa za Boss wake kuchezea mchezo wa bahati nasibu (bettin) na fedha zote Tsh. 190,000 ( Tsh. Mil 3.8) zikaliwa .

Robert ambaye ametoweka tangu November 28,2021 ameacha ujumbe dukani kwa Boss wake ambako amechukua fedha hizo ambapo kwenye ujumbe huo amekiri kutumia fedha za dukani kuchezea bahati nasibu na kusema hiyo ndio sababu ya kukimbia.

Robert alianzia Kituo cha Polisi ambako aliandika maelezo kwa Polisi akikiri kutumia fedha za Boss wake kabla ya kutoweka ambapo aliomba Boss wake apewe shamba lake lililopo Meru kama fidia na aliacha pia simu na nguo zake dukani.

Familia ya Robert inasema kama Robert atabainika kuwa amefariki Kampuni ya betting inapaswa kushughulikia mazishi yake na wakikataa Serikali itapaswa kubeba majukumu hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live