Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomkuta Jamaa aliemtembelea Ex Wake Bila Kumtaarifu, Achomwa kisu

Crime Scene Decoration  Mw 133583 2 Kilichomkuta Jamaa aliemtembelea Ex Wake Bila Kumtaarifu, Achomwa kisu

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: TUKO

< Mwanamme atembelea mpenzi wake wa zamani nyumbani kwake bila kumuarifu na kumkuta na mpenzi wake wa sasaMwanammke huyo apandwa na hamaki, kumdunga kwa kisu na kutoroka na mpenzi wake wa sasaMwanamme huyo amelazwa katika Hosipitali ya Chaani anakoendelea kupata matibabu polisi wakiendeleza msako dhidi ya mshukiwa na mpenzi wakePolisi eneo la Changamwe Kaunti ya Mombasa wanamsaka mwanamke mmoja anayesemekana kumdunga kwa kisu mpenzi wake wa kitambo na kutoroka.

Kwa mujibu wa Chifu wa Kata ya Chaani Ben Baraza mwanamme huyo alikuwa ametembelea nyumbani kwa mpenzi wake wa zamani bila kumuarifu, na kumkuta akiwa na mpenzi wake wa sasa.

Baada ya kuwasili katika nyumba yake, mwanamke huyo anadaiwa kuchukua kisu na kumdunga, akimwacha na majeraha mabaya.

Mhasiriwa alivuja damu kwa kiasi kikubwa lakini majirani majirani walifika na kumkimbiza hospitalini kabla hajaaga dunia.

"Baada ya tukio hilo, mwanamke huyo na mpenzi wake walifunga nyumba na kutoroka na wangali kukamwata," Baraza alisema.

Mwanamme huyo kwa sasa amelazwa katika Hosipitali ya Chaani anakoendelea kupata matibabu huku polisi wakiendeleza msako dhidi ya mshukiwa na mpenzi wake.

Katika kisa sawia, mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 29 anauguza majeraha baada ya kushambuliwa na jamaa aliyemfumania katika chumba chake na mkewe usiku wa kuamkia leo mtaani Donholm, Nairobi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwanamme huyo kwa jina Kangechu alikutana na mwanamke huyo katika sehemu ya burudani na urafiki wao mfupi ukawapeleka nyumbani kwa mwanamke huyo.

"Kangechu na mwanamke huyo walikuwa wanafurahia muda wao, mwanamme huyo alipowafumania chumbani mwake saa kumi alfajiri. Kilichofuta ni makabiliano yaliyomwacha Kangechu na majeraha mabaya," taarifa ya polisi inasema.





Mwanamke huyo anasemekana kupata majeraha madogo katika juhudi za kudhibiti makabiliano hayo.

Mhasiriwa anaendelea kupokea matibabu hospitalini huku mshukiwa akizuliwa na polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO