Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila mtu yuko salama baada ya jengo kuporomoka Nairobi

Kila Mtu Yuko Salama Baada Ya Jengo Kuporomoka Nairobi Kila mtu yuko salama baada ya jengo kuporomoka Nairobi

Wed, 8 May 2024 Chanzo: Bbc

Jengo la orofa tano liliporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumanne usiku na kusababisha operesheni kubwa ya uokoaji, inayoongozwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya.

Jengo hilo liliporomoka huko Uthiru - viungani mwa jiji - huku ripoti za awali zikionyesha kuwa makumi ya watu walikuwa wamenasa chini ya vifusi.

Lakini Jumatano asubuhi Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema wapangaji wote wa jengo hilo wamehesabiwa.

Wengine kumi waliokuwa na majeraha madogo walitibiwa katika eneo la tukio, shirika la misaada liliongeza.

Video kadhaa zilizoshirikiwa mtandaoni zilionyesha jengo la ghorofa likiwa limepinda huku watazamaji wakipaza sauti.

Bramwel Simiyu, afisa mkuu wa usimamizi wa majanga Nairobi, aliondoa hofu ya wakaazi wanne waliotoweka, akiwemo msichana wa miaka 10, akisema wakaazi wote 34 walikuwa wamepatikana na wako salama, tovuti ya habari ya The Star iliripoti.

"Jengo lilikuwa likizama polepole, na wakaazi wote waliweza kuruka na kufanikiwa kutoka nje ya jengo hilo," Bw Simiyu alisema.

Hata hivyo, alisema mbwa wa kijeshi wa kunusa watatumwa ili kubaini ikiwa kuna watu zaidi walionaswa kwenye vifusi.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu Machi ambayo imegharimu maisha ya watu 238 na wengine 235,000 kuyahama makazi yao.

Chanzo: Bbc