Kuwasili kwa vikosi vya Rwanda Agosti 2021, katika eneo la Palma nchini Msumbiji ambalo lilikuwa kituo cha wanamgambo wa Al-Shabaab kwa miezi kadhaa, kumeleta usalama wa kiasi katika eneo hilo, na kuwezesha watu wengi kurejea nyumbani licha ya siku chache zilizopita Umoja wa Mataifa UN, kuonya kwamba mzozo katika eneo hilo bado haujaisha.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda, Luteni-Colonel Ronald Rwivanga amesema, “Matukio ya kawaida tunayopata ni matukio ya pekee, shambulio moja la hapa na pale, watu wachache kwa kweli sio ngome kuu kama ilivyokuwa huko Mocimboa da Praia hata hivyo, tunaweza kusema wakala huyu wameshindwa.”
Eneo hilo, licha ya kutajwa kutumika kwa vitendo vya uasi, havikuzuia vikosi vya Rwanda kuwasili na kuonesha imani katika hali ya usalama ambayo bado ni tete katika eneo hilo lenye utajiri wa gesi huku ikifahamishwa kuwa vikosi vya usalama vya Msumbiji havina mafunzo na vifaa vya kutosha ikilinganishwa na wenzao wa Rwanda.
Amesema, “Awamu inayofuata itakuwa kujaribu kuona kama sekta ya usalama inaweza kufanyiwa mageuzi hadi kufikia hatua ambayo wataweza, watakuwa tayari kukabiliana na usalama baada ya kuondoka kwa kikosi cha usalama cha Rwanda na mwaka mmoja mbele, hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo, na vivyo hivyo na wakazi wengi wa Quionga.”
Wanajeshi wa Rwanda wamezilinda wilaya muhimu za Palma na Mocimboa da Praia zilizopo nchini humo (Msumbiji), ambazo zamani zilikuwa ngome za wanajihadi huku mwalimu wa Kiingereza katika eneo hilo, Jonas Alvaro José, akisema kwassa hali ni nzuri zaidi ikilinganishwa na nyakati zilizopita.
Jonas Alvaro José anaongeza kuwa, “Hivi sasa mambo yamedhibitiwa kidogo na ikilinganishwa na nyuma kwasababu wapo huru na wanafanya chochote ila mzozo huo umeenea katika jimbo jirani la Nampula, ambalo lilipata mashambulizi manne ya makundi yenye silaha mwezi Septemba, yakiathiri takriban watu 47,000 na kuwafanya 12,000 kuyahama makazi yao.”