Maafisa wa ulinzi wa rais wa Afrika Kusini wamekwama katika ndege nchini Polanda kwa saa kadhaa baada ya mamlaka kuwazuia wao pamoja na waaandhi wa habari walioandamana nao kuendelea na safari kuelekea Ukraine ambako Cyril Ramaphosa anaongoza ujumbe wa amani wa viongozi wa mataifa ya Afrika.
Ndege ya kukodishwa ya SAA iliyokuwa na watu 120 imeripotiwa kutua katika uwanjawa ndege wa Chopin mjini Warsaw mapema Alhamisi mchana.
Mkuu wa usalama wa Ramaphosa, Meja Jenerali Wally Rhoode, ilisema serikali ya Poland inahatarisha usalama wa rais kwa kutowaruhusu kuendeklea na safari.
"Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais wetu hatarini," aliwaambia waandishi wa habari. "Kwa sababu tungelikuwa Kyiv kwa sasa lakini wameamua kutufanyia hivi. Nataka mujioneee jinsi walivyo wabaguzi wa rangi."
Mamlaka ya Poland haijatoa maoni yoyote kuhusiana na sualahilo ambalo limegeuka kuwa mzozo wa kidiplomasia - ingawa haijamzuia Bw Ramaphosa mwenyewe kuelekea Kyiv, ambako aliwasili kwa treni Ijumaa asubuhi.
Alipokelewa katika mji mkuu wa Ukraine na balozi wa Afrika Kusini na mjumbe maalum wa Ukraine katika Mashariki ya Kati na Afrika, kulingana na urais wa Afrika Kusini.
Baadaye atasafiri hadi Urusi katika azma ya Afrika ya kusuluhisha mzozo huo.
Mmoja wa wale ambao bado kwenye ndege katika mji mkuu wa Poland ni mwandishi wa habari wa News24 Pieter du Toit, ambaye alichapisha video siku ya Ijumaa asubuhi akisema walikuwa wamekwama kwenye lami kwa karibu saa 24.
"Wafanyakazi wa SAA wamekuwa wakifanya kila juhudisana kumsaidia kila mtu kwenye ndege hiyo.
Hali kwenye ndege hiyo sasa imeanza kufanana na ya kambi ya wakimbizi kwani mahitaji yanapungua," alisema.
"Kikosi cha usalama ambacho kilipaswa kumlinda rais kwenye ziara yake huko Kyiv bado kiko kwenye ndege."