Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi cha UN na jeshi la DRC waanzisha operesheni dhidi ya waasi

Vikosi UN Na Drc.jpeg Kikosi cha UN na jeshi la DRC waanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda usalama kwa kushirikiana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimeanzisha operesheni ya kulinda miji miwili ya mashariki mwa nchi hiyio mbele ya mashambulizi ya waasi wa M23.

Hayo yamesemwa na Stephane Dujarric, msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ameongeza kukwa ujumbe wa kulinda amani, unaojulikana kwa kifupi kwa jina la MONUSCO, jana Jumanne ulitangaza kuanza Operesheni Springbok ya kulinda miji muhimu ya kanda za Goma na Sake, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Amesema: Hatua hiyo ni kujibu mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 na makundi yenye silaha katika jimbo la Kivu Kaskazini pamoja na kusonga mbele waasi wa M23 kuelekea mji wa Sake.

Ameongeza kwa kusema: "Walinda amani wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Kongo wanashika doria katika maeneo muhimu ili kulinda usalama wa watu na kuzuia kusonga mbele zaidi M23,"

Vile vile amesema: "MONUSCO pia imeanzisha maeneo ya ulinzi karibu na kituo cha Kitchanga ili kusaidia kulinda usalama wa watu 25,000 ambao wameomba hifadhi katika kituo hicho kinachojishughulisha na masuala tofauti yakiwemo ya utoaji wa misaada ya kibinadamu."

Maendeo ya mshariki mwa DRC, haswa Kivu Kaskazini, kwa muda mrefu yamekuwa yakishuhudia mashambulizi na vita kutoka kwa makundi ya waasi kama vile M23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live