Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi cha MINUSMA kimemaliza rasmi majukumu yake nchini Mali

Minusma Un Un Kikosi cha MINUSMA kimemaliza rasmi majukumu yake nchini Mali

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Mali (MINUSMA) kimehitimisha rasmi majukumu yake nchini humo baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka kumi. Haya yameelezwa na msemaji wa MINUSMA.

Fatoumata Kaba, msemaji wa kikosi cha MINUSMA amesema kuwa kikosi hicho jana Jumatatu kiliteremsha bendera ya Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya kikosi hicho huko Bamako, mji mkuu wa Mali. Kaba ameongeza kuwa hafla hiyo inaashiria kumalizika rasmi muda wa kuhudumu kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Mali, MINUSMA licha ya kuwa baadhi ya vifaa vyao bado vipo katika makao makuu hayo. Fatoumata Kaba, Msemaji wa MINUSMA

Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Juni mwaka huu serikali ya kijeshi ya Mali iliyotwaa madaraka mwaka 2020 ilitaka kuondoka nchini humo kikosi cha MINUSMA ambacho kiliwasili Mali mwaka 2013 licha ya kukabiliwa na mashambulizi mtawalia ya makundi yenye silaha katika eneo la Sahel.

Kuondoka Mali kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kumeibua hofu juu ya kuanza tena mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na makundi ya wanamgambo wenye silaha kwa ajili ya kuyadhibiti baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kikosi cha MINUSMA kilikuwa na wanajeshi na polisi wasiopungua 15,000 huko Mali katika muongo mmoja wa karibuni. Aidha askari wasioungua 180 wa kikosi hicho wameuawa katika mashambulizi kati yao na makundi ya wanamgambo wenye silaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live