Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi cha MINUSMA chamaliza rasmi majukumu yake nchini Mali

Minusma Kikosi cha MINUSMA chamaliza rasmi majukumu yake nchini Mali

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) kimehitimisha rasmi majukumu yake nchini humo baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka kumi.

Jumapili ya jana, Desemba 31 iliaashiria kumalizika rasmi kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), ambao ulifungasha virago mapema siku ya Jumamosi.

Mwezi Juni mwaka jana (2023) serikali ya kijeshi ya Mali iliyotwaa madaraka mwaka 2020 ilitaka kuondoka nchini humo kikosi cha MINUSMA ambacho kiliwasili Mali mwaka 2013 licha ya kukabiliwa na mashambulizi mtawalia ya makundi yenye silaha katika eneo la Sahel.

Kuondoka Mali kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kumeibua hofu juu ya kuanza tena mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na makundi ya waasi kwa ajili ya kuyadhibiti baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kikosi cha MINUSMA kilikuwa na wanajeshi na polisi wasiopungua 15,000 huko Mali katika muongo mmoja wa karibuni. Aidha askari wasioungua 180 wa kikosi hicho wameuawa katika mashambulizi kati yao na makundi ya wanamgambo wenye silaha.

Maafisa wa Mali wanaamini kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo umefeli katika jukumu lake. Wan asema, uwepo wa vikosi vya "Minusma" nchini Mali umekuwa kazi bure. Kugunduliwa makumi ya makaburi ya umati, mauaji ya raia na kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi nchini Mali na nchi nyingine jirani ni miongoni mwa sababu zinazoashiria kushindwa jeshi la Ufaransa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live