Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi cha EACRF chaweka mkakati wa kudumishwa kwa amani DR Congo

Kikosi Cha EACRF Chaweka Mkakati Wa Kudumishwa Kwa Amani DR Congo Kikosi cha EACRF chaweka mkakati wa kudumishwa kwa amani DR Congo

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Kikosi cha Jumuiya ya Mashariki kinachokamilisha hatua za kuondoka mashariki mwa DRC kinasema kwamba kimefanya mipango muhimu ya kuhakikisha kikosi cha muungano wa kimaendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika SADC kinachotarajiwa kuingia unaendeleza majukumu ya kudimisha amani bila ya hitilafu.

Akizungumza mjini Goma, mapema alahamisi hii, mkuu wa kikosi cha EACRF Meja Jenerali Alphaxard Kiugu ametaja pia kwamba japo EACRF iliweza kuhakikisha kwamba hali ya kusitishwa kwa mapigano iliyoafikiwa kati ya makundi ya wapiganaji yakiongozwa na kundi la M23 na serikali ya DRC, kwa muda kati ya Machi 7 na Oktoba 7 mwaka huu, hali ya kuvunjika kwa makubaliano hayo na kurejelewa kwa mapigano linatia wasiwasi kuhusu usalama wa jimbo la Kivu kaskazini.

‘Kuwepo kwa makundi ya wapiganaji yanayojipanga kuingia katika maeneo ambayo vikosi vya EACR vimeondoka, kurejea kwa kishindo makundi ya wapiganaji katika maeneo ambayo ni makazi ya raia, mapigano kati ya makundi hayo ya wapiganaji, na taarifa za propaganda dhidi ya kikosi cha EAC ni baadhi ya masuala yanayorejesha nyuma mafanikio ambayo yalipatikana katika muda ambao kikosi kimehudumu,’alisema Jenerali Kiugu katika kikao cha wanahabari mjini Goma.

Kikosi hicho kimeshutumiwa kwa kukosa kutekeleza jukumu kuu la kukabiliana na kundi la M23 ambalo uongozi wa juu wa DRC ulikisisa kwamba EACRF ilishirikiana na wala kutodhibiti kundi la M23.

Katika kikao cha viongozi wa EAC mapema mwaka huu nchini Burundi, Rais Tsishekedi alionekana kumkemea aliyekuwa mkuu wa kikosi cha EACRF Meja Jenerali Jeff Nyagah kwa hali aliyohisi ni muongozo aliodhania EAC utatumia kudhibiti usalama mashariki mwa DRC kutofuatwa.

Hali imekuwa ngumu kwa kikosi hicho mwaka huu ambapo maandamano kupinga kuwepo kwa kikosi hichon yameandaliwa mjini Goma mara kadhaa, huku raia wakieleza pia kughadhabishwa na walichokitaja kuwa hali ya wao kutatizika japo kuna vikosi vya kijeshi vilivyotumwa huko kujukumia suala la usalama.

Chanzo: Bbc