Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikao cha Umoja wa Afrika chalaani wimbi la mapinduzi

AU MAPINDUZI Kikao cha Umoja wa Afrika chalaani wimbi la mapinduzi

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika umelaani wimbi la mapinduzi ya hivi karibuni ambalo limeshuhudia idadi kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa ya nchi wanachama zikisimamishwa kutoka umoja huo.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa baraza la amani na usalama wa Umoja huo Bankole Adeoye wakati kikao cha kila mwaka cha Umoja huo kikikaribia kumalizika.

Adeoye amewaambia wanahabari kwamba kila kiongozi wa Afrika katika baraza hilo amelaani wimbi hilo la mabadiliko ya serikali kinyume na katiba.

Mataifa manne wanachama yalisimamishwa uanchama wao katika Umoja huo tangu katikati ya mwaka 2021 kwasababu ya mabadiliko ya serikali kinyume na katiba .

Mapinduzi ya hivi karibuni zaidi yaliotokea nchini Burkina Faso, ambapo wanajeshi walimuondoa madarakani rais Roch Marc Christian Kabore mwezi uliopita.

Adeoye aliwataka wanahabari hao kufanya utafiti akisema hakuna wakati katika historia ambapo Umoja wa Afrika ulisimamisha uanachama wa mataifa manne ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, akimaanisha Mali, Guinea, Sudan na Burkina Faso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live