Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana wa miaka 22 aliyepora Benki zaidi ya Tsh. Milioni 900 akamatwa

De40d22b6ba13d42 Kijana wa miaka 22 aliyepora Benki zaidi ya Tsh. Milioni 900 akamatwa

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Makachero wa DCI wamemtia mbaroni kijana wa miaka 22 ambaye anahusika na kupora mabenki mamilioni akitumia teknolojia.

DCI walifaulu kumkamata Kipkemoi ambaye anahusishwa na genge ambalo linawapora wateja wa mabenki fedha bila huruma. Kijana huyo Alikuwa katika maficho huko Narok ambapo DCI walisema alikuwa akipunga upepo baada ya kuwapora Wakenya KSh 45M.

Mshukiwa huyo na kundi lake wamekuwa wakilenga Wakenya ambao wanatumia simu zao kuweka au kutoa fedha katika akaunti.

Kwa mujibu wa DCI, kijana huyo amekuwa akinyemelea akaunti za Wakenya ambapo hufyonza fedha bila ya wao kujua.

Kufikia kukamatwa kwake, DCI wanasema alihusika na kupora takriban KSh 45M kutoka benki moja tajika humu nchini.

DCI walisema Nelson Kipkemoi alipatwa katika pango lake eneo la Mulot Narok ambapo amekuwa akiendesha njama ya kunyonya fedha kutoka akaunti za wateja bila wao kujua.

“Nelson Kipkemoi, 22, amekamatwa na makachero wa kukabiliana na uhalifu wa mabenki katika maficho yake Mulot, kaunti ya Narok leo alasiri baada ya kuhusishwa na genge linalowalaghai wateja wa benki kwa kufyonza fedha kutoka akaunti zao,” taarifa ya DCI ilisema.

Inaarifiwa genge hilo limewapora wateja 481 na hulenga wale ambao hutumia mfumo wa simu kuweka au kutoa fedha kwenye akaunti zao.

“Amekuwa akilenga akaunti za Wakenya 481 ambao wako kwenye benki moja maarufu humu nchini na wale wanaotumia simu kuendesha shughuli za akaunti zao,” DCI iliongeza.

Kipkemoi atafikishwa mahakamani hii leo na kushtakiwa huku uchunguzi ukiendelea ili kuwafichua walioshirikiana naye.

Wakenya wengi wamekuwa wakilia kuhusu akaunti zao kuibwa fedha huku mabenki nchini yakisalia kimya kwa hofu ya kuharibu jina kwenye biashara.

Mjini Nakuru, polisi wamekuwa wakikabiliana na kundi hatari la Confirm ambalo hutumia ujanja kuwalaghai Wakenya kwa kutoa fedha kwenye mtambo wa Mpesa.

Kundi hilo hutumia ujanja kama vile kudai wamekutumia pesa kimakosa na hivyo kukutaka uwarejeshee.

Mbinu nyingine huwa kukufunga macho kwa maelekezo kwenye simu yake kiasi kwamba unaishia kusambaza fedha kwa wao.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke