Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana wa DRC mwenye kipaji cha kujigeuza kuwa sanamu

Fe778390 Db86 11ee 86d7 F1795935a538 Kijana wa DRC mwenye kipaji cha kujigeuza kuwa sanamu

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mayanda Nzau, maarufu "Mutu Ekeko" (Mtu Sanamu), amejizolea umaarufu mkubwa katika Jiji la Kinshasa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kutoka na uwezo wake wa kujigeuza kuwa kama sanamu.

Kijana huyu mwenye umri wa miaka 31 baada ya kujisaidia haja kubwa na ndogo asubuhi, anaweza kusimama kwa muda wa saa kumi bila kujitikisa na kuwaacha watu wakibishana kama ni mtu au la.

Kipaji chake hicho alichoanza kukiibua akiwa chuo kikuu kwa kuigiza sanamu lililokuwa getini chuoni hapo, kimempa ajira mbali na kualikwa kwenye matukio mbalimbali zikiwemo dhifa za kitaifa nchini mwake.

Mayanda, ameajiriwa na Idara ya Serikali ya Makumbusho na kwa sasa yeye ni moja ya vivutio muhimu!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live