Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana aliyeacha shule kwa kukosa ada abuni gari

Homa Bay Man Makes First Car In Nyanza Kijana abuni gari

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipaji ni kitu ambacho watu wengi wamejaaliwa kuwa nacho ila ni watu wachache huwa wanafanikiwa kugundua vipaji vyao nakuvifanyia kazi mpaka wanafanikiwa

Kijana mmoja kutoka Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya anayetambulika kwa jina la Bernard Otieno Ochieng, ameshangaza watu kutokana na kipaji chake na uwezo wa ubunifu baada ya kubuni gari lake la siti mbili za kukaa.

Mwaka 2010, Ochieng aliacha shule baada ya kushindwa kulipa karo, baada ya hapo alianza kujifunza ufundi wa magari kwa sababu ni kitu ambacho alikuwa anakipenda tangu akiwa shule. Kipindi yupo shule alikuwa anapenda kutumia computer kuangalia mtandaoni jinsi magari yanavyoundwa na kujifunza.

“Nilikuwa na ndoto ya kujiunga na chuo kikubwa cha ufundi, ili nisome nije kuajiriwa na kampuni kubwa za kutengeneza magari. Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikitengeneza magari kwa kutumia vifaa vya kienyeji," amesema Ochieng.

Ochieng anasema alishawishiwa kwa kutazama michoro ya magari kupitia vitabu na kwenye computer jambo lililompa nguvu na ari ya kuanza kuchora gari analolitaka kabla ya kuanza kulitengeneza.

“Ninapima uzito wa mataili, una urefu kujua wapi nitaweka injini na wapi bodi likae ili kutosababisha msuguano. Gari yangu haijazibwa juu (iko wazi) na inabeba watu wawili.

Amesema kwa sasa anawekeza katika kutenegeneza ndege ndogo na gari ndogo kwa ajili ya watoto wake.

“Nikiwa ni mtaji na vifaa nitatengeneza gari kubwa na zuri zaidi. Nina ndoto ya kufanya kazi na makam[puni makubwa hapa nchini na nje ya nchi kutimiza hiki nilichokianza," amesema Ochieng.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live