Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana ajiua kisa Mungu hajajibu maombi yake

UDS STUDENT Alfa Musa.

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi wa masomo ya Kiarabu amejiua kwa madai Mungu hajamjibu maombi yake. Alfa Musa (22) toka nchini Nigeria alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sheikh Kamaldeen ya masomo ya Kiarabu.

Desemba 7, mwaka huu, mlango wa chumba cha mwanafunzi huyo ulikutwa umefungwa kwa ndani na ulipovunjwa alikutwa amejiua mwili wake unaning'inia huku akiwa ameacha ujumbe wa kuwaomba msamaha wazazi wake kwa uamuzi aliochuukua, amedai amejiua sababu Mungu hajamjibu maombi yake.

Amedai ni bora kujiua kuliko kutenda dhambi na kuomba akazikwe kwao. Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kujaribu kufanya uchunguzi zaidi, hata hivyo tayari amezikwa na baadhi ya wanafunzi wenzie kushea picha za mazishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live