Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiira Motors kuzalisha magari ya umeme 5000

Kiira Kiira Motors Uganda

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya magari ya Kiira ya Uganda inayotengeneza vipuri vya magari na magari imefanikiwa kuzalisha theluthi mbili ya vifaa vya magari ambavyo kufikia mwaka 2030 inalenga kuanza rasmi uzalishaji kwaajili ya biashara.

Katika kuelekea mwaka 2030 tayari kampuni ya magari ya Kiira imezalisha vipuri vipatavyo 19500 kati ya 30,000 ambavyo vimezalishwa ndani ya nchi ya Uganda.

Uzalishaji wa vipuri vya magari huko Jinja umekalimika kwa asilimia 85% na uzalishaji kwaajili ya biashara unatarajia kuanza mwaka 2022 lengo likiwa ni kukamilisha magari 5000 kwa mwaka. Baada ya mwezi mmoja mabasi 300 yanayotumia nishati ya jua na nishati ya umeme yanatajwa kukamilika na kupelekwa mjini Kampala.

Agosti 14 mwaka huu Rais Yoweri Museveni aliongoza hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kiwanda hicho ambapo kiwanda kiliweka wazi mpango wake wa uzalishaji na usambazaji.

Kampuni ilidai kupungukiwa na dola milioni 40 kwaajili ya kununua vifaa vya kutengenezea, fedha ambazo zinatakiwa kutoka kwenye mapato ya ndani. Hadi sasa kampuni imetengeneza mabasi matatu na mengine bado yanasubiri kumaliziwa baadhi ya sehemu katika kituo kingine cha utengenezaji cha Nakasongola.

Hivi karibuni Mtendaji mkuu wa Rais Museveni na Rais Museven walizuia uagizwaji wa baadhi ya vifaa vya kutengenzea mabasi na malori kutoka nje.

"Hakutakuwa na mabasi yanayotengenezwa kwaajili ya biashara ndio sera tunayokuja nayo. Kwa sasa tunataka baadhi ya vipuri na spea viagizwe nje lakini tunahitaji vipuri kama spea muhimu zitengenezwe ndani". alisema mkuu huyo.

Rais Museben alisema Uingizwaji wa vifaa vya magari vilivyotumika pia vitazuiliwa kwa sasa ili kuruhusu matumizi ya spea zinazozalishwa ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live