Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiir wa Sudan Kusini aahidi uchaguzi wa kwanza nchini humo

Kiir Wa Sudan Kusini Aahidi Uchaguzi Wa Kwanza Nchini Humo Kiir wa Sudan Kusini aahidi uchaguzi wa kwanza nchini humo

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, Jumanne ameahindi kwamba uchaguzi uliocheleweshwa uliopangwa kufanyika mwaka ujao utaendelea kama ilivyopangwa na kwamba atawania urais.

Kiir, ambaye ni kamanda mkuu wa wapiganaji wa msituni, amekuwa rais pekee wa taifa hilo tangu alipoliongoza kupata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011.

Kipindi cha mpito kilikusudiwa kuhitimishwa na uchaguzi mnamo Februari 2023, lakini serikali hadi sasa imeshindwa kufikia vifungu muhimu vya makubaliano, ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba.

"Ninakaribisha uidhinishaji wa kugombea urais mwaka 2024," Kiir aliwaambia wafuasi wa chama chake tawala cha Sudan People's Liberation Movement, akilielezea kama "tukio la kihistoria."

Hasimu wa Kiir Riek Machar(kulia) anatarajiwa kugombea urais katika uchaguzi ujaoImage caption: Hasimu wa Kiir Riek Machar(kulia) anatarajiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao Hakuna mgombea mwingine ambaye ametangaza kugombea, lakini adui wa kihistoria Riek Machar anatarajiwa kugombea.

Mwezi Agosti, viongozi hao wawili waliongeza serikali yao ya mpito kwa miaka miwili zaidi ya muda uliokubaliwa, wakitaja haja ya kushughulikia changamoto zilizokwamisha utekelezaji wa makubaliano ya amani.

Chanzo: Bbc