Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiir atunukiwa medali ya amani

1626023f8e941267f549b86d1cb2d915 Kiir atunukiwa medali ya amani

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Amani bila Mipaka Duniani limemtunuku Rais Salva Kiir medali ya amani kwa mwaka 2020 kutokana na juhudi zake za kuleta amani.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais imesema kuwa, Rais Kiir ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na mikakati yake ya kuleta amani kwa watu wa Sudan Kusini na Sudan.

Tuzo hiyo imewasilishwa kwa Rais Kiir na Dk Muhammad el-Arab kutoka Taasisi ya Amani bila Mipaka kwa ufadhili wa nchi za Gulf ikiwamo Qatar, Saudi Arabia na Bahrain.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa nchi hizo za Gulf zimetambua juhudi za Rais Kiir kama mtu wa amani ambaye anastahili kutambuliwa na kamati ya utoaji tuzo hiyo.

Shirika la Amani bila Mipaka Duniani linatoa tuzo hiyo kwa viongozi waliochaguliwa ambao wameonesha juhudi katika kuleta amani ama kwa nchi zao au nchi jirani.

Shirika hilo limempongeza Rais Kiir kwa jukumu muhimu ambalo ameendelea kutekeleza kujadili amani na kupatanisha watu wa Sudan na Sudan Kusini.

Baada ya kumpa Rais Kiir medali hiyo, mataifa ya Ghuba yaliahidi nia yao ya kuimarisha uhusiano na nchi hizo mbili za Sudan Kusini na Sudan.

Dk Muhammad el-Arab alisema nchi za Ghuba zinatarajia kufungua ofisi ya ubalozi nchini Sudan Kusini na ubalozi wa Bahrain huko Juba.

Hii ni tuzo ya pili kwa Rais Kiir kupokea chini ya miezi mitatu mwaka huu kwa juhudi zake za keleta amani.

Chanzo: habarileo.co.tz