Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiingereza chawakosesha kazi wauguzi Kenya

Test Kiingereza chawakosesha kazi wauguzi Kenya

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe amebainisha sababu kuu iliyopelekea watumishi wa afya nchini humo kufeli mtihani wa kiingereza ulioandaliwa kwaajili ya kupata nafasi za kazi nchini Uingereza.

Waziri huyo amesema kuwa wauguzi hao wameshindwa kufaulu mtihani wa kiingereza kwa kukosa uelewa thabiti wa lugha hiyo hivyo kupoteza nafasi za kazi ambazo zilitangazwa katika mpango mpya wa Kenya na Uingereza.

"Kati ya wauguzi 300 waliofanya mtihani wa kiingereza ni 10 pekee ndio wamefaulu, tuliingia makubaliano na Uingereza kwa ajili ya kutupatia nafasi za kazi lakini matokeo yamekuwa mabaya sana na bahati sio yetu" Amesema Waziri huyo.

Ameongeza kusema kuwa mbali na matokeo hayo bado Serikali itaendelea kufanya mikakati ya ajira kwa waaguzi hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live