Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo ajiengua kuwania Urais DRC

Kuraaa.png Kigogo ajiengua kuwania Urais DRC

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Mstaafu wa DR Congo, Augustin Matata Ponyo amejiondoa kutoka kwenye uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi ujao na kutangaza kumuunga mkono Moïse Katumbi, mfanyabiashara tajiri na aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Katanga.

Wawakilishi wa vyama vikuu vya upinzani nchini DR Congo walifanya mazungumzo mapema wiki hii kuhusu jinsi ya kuhakikisha uchaguzi utakuwa wa haki, na kuchunguza uwezekano wa kuwa na mgombea wa pamoja wa kuwania nafasi ya urais dhidi ya Rais Felix Tshisekedi.

Ponyo anasema anaamini wapinzani wengine watafuata nyayo zake na kujiondoa kwa kumuunga mkono Katumbi dhidi ya Tshisekedi anayewania kwa muhula wa pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live