Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Nigeria afikishwa mahakamani kwa kuuza viungo vya mtoto

Kigogo Nigeria Kigogo Nigeria afikishwa mahakamani kwa kuuza viungo vya mtoto

Fri, 24 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Seneta mmoja wa Nigeria na mkewe wamebainika kama wanandoa waliofikishwa mahakamani kwa kula njama ya kumsafirisha mtoto hadi Uingereza ili kuuza viungo vykae. Msemaji wa Ike Ekweremadu alithibitisha kwa BBC Igbo kwamba seneta huyo alishtakiwa nchini Uingereza kuhusu kesi hiyo.

Wakili huyo mwenye umri wa miaka 60 na mwanasiasa amekuwa Seneta tangu mwwaka 2003 na ni mwanachama wa chama cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP).

Alihudumu kwa mihula mitatu kama naibu rais wa Seneti wa Nigeria kutoka 2007 hadi 2019. Mkewe, Beatrice Nwanneka Ekweremadu, anatarajiwa kujitokeza naye baadaye katika Mahakama ya Uxbridge nchini Uingereza kujibu mashata hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live