Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiambaa: Uhuru na DP Ruto wafungulia mifereji kutafuta ushindi wa uchaguzi mdogo

4ee19cf4a43f86ae Kiambaa: Uhuru na DP Ruto wafungulia mifereji kutafuta ushindi wa uchaguzi mdogo

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiambaa imebadili methali ya wanapopigana fahali wawili kwani badala ya nyasi kuumia ndio inafaidika sasaUhuru na Ruto wamefungulia mifereji na sasa wakazi wanaonja utamu wa mifuko yao mizitoKila upande wa kisiasa unatafuta kiti cha ubunge eneo hilo kwa bidii na hivyo kuwekeza kila mbinu ili kupata ushindiImekuwa ni hali ya mgeni njoo mwenyeji apone katika eneo bunge la Kiambaa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika Alhamisi.

Vyama vya United Democratic Alliance (UDA) na Jubilee vimepiga kambi katika eneo bunge hilo kila pande ikiwarai wakazi kupiga kura kwao.

Ni hali ambayo iligeuza wakazi hao na kuwa kama kipusa mrembo kwenye mtaa anayesakwa na kila dume.

Hilo limefanya kila upande kujikakamua na hivyo wakazi kufaidika pakubwa kutokana na minofu ya kisiasa ambapo mifereji ya asali na maziwa hufunguliwa.

Habari Nyingine: Caroline Kangogo Alikuwa Katika Kundi la Wezi wa Kimabavu Bonde la Ufa

Ushindani ni mkali kati ya wagombea Njuguna Wanjiku wa UDA na Kariri Njama wa Jubilee huku vigogo wa kisiasa wakitua humo kurai wakazi kujitokeza Julai 15 kupigia mgombea wao kura.



Read also

Mtahiniwa wa KCSE Ajitoa Uhai Baada ya Kuandikia KNEC Barua

Uchaguzi huo ni muhimu sana kwa vyama vyote viwili kwani unaonekama kama vita kati ya Naibu Rais William Ruto na mdosi wake Uhuru Kenyatta.

Kutokana na uhusiano baridi wa kisiasa kati ya wawili hao, wanapimana nguvu ni nani ana usemi katika siasa za Mt Kenya.



Wote wawili wametuma makamanda wao kupiga kambi humo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Tofauti na msemo wa fahali wawili kupigana ambapo nyasi huumia, kwenye kisa cha Kiambaa imekuwa ni faida kwao.

Makamanda waliotumwa kupigana vita vya vyama vyao wamejihami kwa mifuko mizito na meza ya TUKO.co.ke imepata habari kuwa fedha zinatolewa kwa wingi kwa wapiga kura.

Katika video moja inayosambaa kwenye mtandao, wakazi wanaonekana wakiwa kwenye foleni ambapo wanapokezwa michuzi na vyakula.



Read also

Caroline Kangogo Alikuwa Katika Kundi la Wezi wa Kimabavu Bonde la Ufa

Wadadisi wa kisiasa wanasema ingali ngumu kujua ni nani ataibuka mshindi kwenye kivumbi hicho kikali ila tu kusubiri debe Alhamisi Julai 15.

Kura hiyo itaonyesha wakazi watakuwa wamemcheza nani ambaye wamekula mali yake lakini kura waweke pengine.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke