Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya mipaka Kenya na Somali kaa la moto

Kenyatta Pic Dataeded Kesi ya mipaka Kenya na Somali yapamba moto

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ICJ wa kuipatia Somalia eneo kubwa la bahari ya Hindi linalogombaniwa kutoka pwani ya nchi hiyo na kutahadharisha kuwa hatua hiyo itatia dosari uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Kenyatta amepinga vkali maamuzi hayo kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi na kusema kuwa maamuzi hayo yatachochea vita za kisiasa na kiuchumi jambo ambalo linatishia usalama katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.

Awali Rais wa Somalia Mohammed Abdullah Mohammed aliitaka Kenya kuheshimu sheria ya kimataifa baada ya Mahakama hiyo kukabidhi umiliki wa eneo hilo kwa Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live