Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya mbunge kumpiga risasi DJ, dhamana ya Babu Owino yapunguzwa

97810 Babu+pic Kesi ya mbunge kumpiga risasi DJ, dhamana ya Babu Owino yapunguzwa

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi. Mahakama Kuu nchini Kenya imepunguza masharti ya dhamana ya Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino kutoka Sh10 milioni hadi Sh 5 milioni za Kikenya kwenye kesi inayomkabili ya kujaribu kumuua DJ Evolve. Jaji Luka Kimaru wa mahakama hiyo wakati akitoa uamuzi  leo Jumanne Machi 03, 2020 amesema washtakiwa  wameshindwa kutoa sababu yoyote kwanini vifungu vya dhamana havipaswi kupitiwa. Babu Owino, ambaye jina lake halisi ni Paul Ongili, alikuwa ameachiwa kwa dhamana  ya Sh10 milioni Januari 27, 2020 ambapo sasa dhamana hiyo imepunguzwa hadi Sh 5 milioni. Katika uamuzi wa zamani wa Hakimu Mkazi Mkuu wa Milimani, Francis Andayi mahakama ilisema pesa hizo zitatumika kulipa madeni ya hospitali ambayo amelazwa DJ Evolve ambaye jina lake halisi ni Felix Odhiambo Orinda aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na mbunge huyo. Mbunge huyo alikamatwa baada ya tukio la kumpiga risasi DJ Evolve tukio ambalo lilitokea eneo la Club B katika barabara ya Galana, Nairobi nchini Kenya mwezi Januari.

Chanzo: mwananchi.co.tz