Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya mauaji ya kiongozi wa Burkina Faso yaanza kusikilizwa

Sankara In Paris Thomas Sankara Aliyekuwa Rais wa Burkina Faso

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya mauaji ya Thomas Sankara, "baba wa mapinduzi" nchini Burkina Faso inatarajiwa kuanza Oktoba 11, 2021 ikiwa ni miaka 34 tangu kutokea kwa mauaji hayo.

Jumla ya watuhumiwa 14 wanashtakiwa kuhusika katika mauaji hayo akiwemo Rais wa zamani wa nchini hiyo Blaise Compaoré.

Kesi hii ni miongoni mwa kesi zinazosubiriwa kwa shauku zaidi barani Afrika, maelfu ya watu wanasubiri kusikia maamuzi yatakayofikiwa na Mahakama ya kijeshi nchini humo kufuatia mauaji hayo yaliyohusisha vifo vingine 12 vya wafuasi wa kiongozi huyo.

Sankara aliingia madarakani mnamo mwaka 1983, alikuwa na wafuasi wengi sana katika taifa hilo waliokubali sera na aina ya siasa alizokuwa akifanya, alisifika zaidi pale alipokataa kupokea msaada wa kifedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, alisidia kuleta usawa wa kijinsia kwa kutoa nafasi sawa kwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi, alipiga marufuku ndoa za lazima, mitara pamoja na ukeketaji.

Aliuawa miaka 4 baada ya kuingia madarakani, mara baada ya vikosi vya kijeshi kuvamia makao makuu ya chama chake cha National Revolutionary Council, na kumpiga risasi iliyopelekea mauti yake, kisha kumtangaza Blaise aliyekua mtu wa karibu sana na Sankara kuwa Rais wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live