Mahakama kuu ya Milimani inaendelea kusikiliza kesi ya mauaji ya Marehemu aliyekuwa mbunge wa Kabete George Muchai.
Kesi hiyo imekuwa ikiendelea tangu Jumatatu na inatarajiwa kuendelea hadi Ijumaa.
Afisa mpelelezi amepandishwa kizimbani akitoa ushahidi wake kuhusiana na kesi hiyo.
Wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni Eric Isabwa almaarufu Chairman, Raphael Kimani almaarufu Kim Butcher, Mustapha Kimani almaarufu Musto, Stephen Astiva almaarufu Chokore, Jane Wanjiru almaarufu Shiro, Margaret Njeri na Simon Wambugu.
Wamekanusha mauaji ya mbunge huyo wa zamani, walinzi wake wawili na dereva.
Marehemu George Muchai aliwauawa tarehe 7, mwezi Februari mwaka 2015 pamoja na wasaidizi wake kwa kupigwa risasi nyakati za usiku.