Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kihistoria ya Ousman Sonko yaibua matarajio mengi

Sonko Gambia Gambia.png Kesi ya kihistoria ya Ousman Sonko yaibua matarajio mengi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya kihistoria ilifunguliwa siku ya Jumatatu, Januari 8 nchini Uswisi. Kutokana na kanuni ya mamlaka inayotumiwa duniani kote, Mahakama ya Shirikisho ya Jinai inamsikiliza Ousman Sonko wa Gambia, afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika utawala wa kidikteta wa Yahya Jammeh. Jumatatu hii, mazungumzo ya kwanza kai ya mawakili yameanza.

Afisa katika ngazi ya juu kama hii ya uongozi hajawahi kuhukumiwa barani Ulaya chini ya kanuni ya mamlaka inayotumiwa duniani kote. Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ulinzi wa rais, wakati huo inspekta jenerali wa polisi na hatimaye Waziri wa Mambo ya Ndani kwa miaka kumi chini ya udikteta wa Yahya Jammeh, Ousman Sonko anatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, mateso, utekaji nyara na hata kunyongwa bila ya mahakama. Alitoroka Gambia mwaka wa 2016 kabla ya kukamatwa nchini Uswisi mwaka uliofuata. Kesi hii kwa hivyo inaahidi kuweka historia wakati hapo awali, ni uhalifu mmoja tu kutoka enzi ya Yahya Jammeh ambao umehukumiwa duniani.

Kulingana na wakili Reed Brody, wa tume ya kimataifa ya wanasheria, Ousman Sonko alikuwa "nguzo ya utawala. Alishiriki katika uhalifu muhimu zaidi." Kulingana na yeye, waziri huyo wa zamani alitumia ukandamizaji, alitoa maagizo ya kuwashambulia watu wasiokuwa na hatia, kuteswa na kubakwa. Lakini pia ana husishwa moja kwa moja na mauaji, anasema Reed Brody, ambaye anatarajia mengi kutoka kwa kesi hii. "Nimejawa na hasira na maumivu"

Kufunguliwa kwa kesi hiyo siku ya Jumatatu kulitoa nafasi kwa mazungumzo ya kwanza kati ya mawakili. Mawakili wa walalamikaji walisisitiza kwamba mashitaka ya unyanyasaji wa kijinsia yaongezwe kwa baadhi ya makosa, hasa mateso na kufanyia watu ukatili wa kuwawekea umeme kwenye sehemu za siri. Kwa mfano, mwanamke ambaye anadaiwa kuwa mtumwa wa ngono na kubakwa angalau mara 60 anatarajia kutoa ushahidi. Pia waliomba makosa makubwa yazingatiwe kutokana na idadi ya waathiriwa na asili ya uhalifu.

Kwa upande wa mshtakiwa, wakili wake alipinga mamlaka ya mahakama kwa ajili ya vitendo vilivyotendwa kabla ya marekebisho ya kanuni ya adhabu ya Uswisi ya mwaka 2011. Pia aliomba kuondolewa kwa baadhi ya shahidi na vielelezo, visivyokubalika kulingana na wakili huyo.

Mwanahabari Madi Ceesay alikuwa akisubiri kuanza kwa kesi hiyo. Alikamatwa na kuteswa wakati Ousman Sonko alipokuwa inspekta jenerali wa polisi. “Hili ni muhimu kwangu kwa sababu ninatumai kuwa hivi karibuni nitapata haki. Nimekuwa nikingojea siku hii kwa muda mrefu. Nimejawa na hasira na maumivu. Natumai majaji watanipa ahueni. Nasubiri ukweli usikike na haki itendeke,” amesema.

Kesi ya Ousman Sonko inatarajiwa kudumu kwa angalau wiki tatu na inaweza kuhimiza vyombo vya sheria nchini Gambia ambapo hakuna uhalifu uliotendwa chini ya Yahya Jammeh ambao umehukumiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live