Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Uchaguzi Kenya: Magari yazuiwa kupita eneo la mahakama

Kenya Kmm.jpeg Kesi ya Uchaguzi Kenya: Magari yazuiwa kupita eneo la mahakama

Sun, 4 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katazo hilo linakuja ikiwa ni masaa chini ya 24 yamesalia kwa Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu Matokeo ya Rais ambayo yaliwekewa Pingamizi na Mgombea wa Azimio, Raila Odinga.

Katika taarifa yake Jeshi la Huduma za Polisi (NPS) pia limezuia matumizi ya Barabara zote zinazoelekea katika Mahakama Kuu ambazo zitafungwa ili kuepusha mikusanyiko kwenye jengo hilo wakati wa kutolewa uamuzi wa Majaji

Ijumaa Septemba 2,2022 Mahakama Kuu ilihitimisha kusikiliza Pingamizi hilo na inatarajiwa kurejea tena Jumatatu Sept. 5,2022 kwa ajili kutoa uamuzi wa kamati ya Majaji 7 inayoongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live