Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Maafisa wa Misri kuua mwanafunzi wa Kiitaliani yaahirishwa tena

Kesi Ya Maafisa Wa Misri Kuua Mwanafunzi Wa Kiitaliani Yaahirishwa Tena Kesi ya Maafisa wa Misri kuua mwanafunzi wa Kiitaliani yaahirishwa tena

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: Voa

Kesi ya maafisa wanne wa Misri wanaotuhumiwa kumteka nyara na kumuua mwanafunzi wa Kiitaliani huko Cairo imeanza tena Rome siku ya Jumanne, miaka miwili na nusu baada ya kusikilizwa kwa mara ya mwisho, na mawakili wa upande wa utetezi kwa mara nyingine wakitaka kesi hiyo itupiliwe mbali.

Giulio Regeni, mwanafuzi wa shahada ya pili katika chuo cha Cambridge, Uingereza, alitoweka katika mji mkuu wa Misri Januari 16. Mwili wake ulipatikana takribani wiki moja baadaye, uchunguzi wa maiti ulionyesha alikuwa ameteswa kabla ya kifo chake.

Waendesha mashitaka wa Kiitaliani wanawatuhumu maafisa wanne wa Misri kuhusika na mauaji , lakini walishindwa kuwapata ili kuwapa hati ya kufika mahakamani. Matokeo yake wanahukumiwa bila kuwepo mahakamani.

Kesi ilifunguliwa Oktoba 2021, lakini kwa haraka ilisimamishwa baada ya jaji kukubali hoja kutoka mawakili wa utetezi waloteuliwa na mahakama kwamba kesi haitokua na maana endapo hakuna ushahidi kwamba washitakiwa walijua kwamba wameshitakiwa.

Waendesha mashitaka walikata rufaa ya uamuzi huo na mahakama ya juu ya Italia ilifuta malalamiko hayo ya mwaka jana , wakisema Misri kushindwa kushirikiana kuwatafuata washukiwa kusiwe kipingamizi cha kesi hiyo.

Jumanne, mawakili upande wa utetezi walidai kesi hiyo ibatilishwe. Wakisema kuwa haijabainika kama washukiwa bado wako hai na kuhoji kama walitambuliwa kwa usahihi. Mahakimu watatafakari juu ya ombi hilo na keshi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Machi 18.

Chanzo: Voa