Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi kuhusu jaribio la kumuua rais wa Burundi yasikilizwa faraghani

Kesi Kuhusu Jaribio La Kumuua Rais Wa Burundi Yasikilizwa Faraghani Kesi kuhusu jaribio la kumuua rais wa Burundi yasikilizwa faraghani

Tue, 28 May 2024 Chanzo: Bbc

Katika kesi hiyo yake iliyoanza Jumatatu Waziri mkuu wa zamani wa Butundi Alain-Guillaume Bunyonyi anakabiliwa na mojawapo ya uhalifu mkubwa ambao ni kujaribu kumuua mkuu wa nchi kwa njia uchawi. Kesi yake imesikilizwa kwafaragha.

Wanaofuatilia kesi hii wanasema uhalifu na mipango ya kupindua serikali ndiyo msingi wa kesi hii, na wanakosoa kuwa kesi hiyo haijaendeshwa wazi.

Bunyoni ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza alishtuhumiwa kwa makosa saba yakiwemo ya kuhatarisha mali ya nchi, ufisadi, kumiliki silaha bila leseni na uhalifu mwingine.

Mnamo tarehe 12 mwaka jana, Bunyoni alihukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini alikana mashtaka dhidi yake.

Chanzo: Bbc