Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ambapo Moses Kuria alimshambulia mwanamke yafutiliwa mbali na mahakama

68e6ad92e69f4cd1 W Kesi ambapo Moses Kuria alimshambulia mwanamke yafutiliwa mbali na mahakama

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mbunge wa Gatundu Moses Kuria alikuwa ameshutumiwa kwa kumshambulia Wanja wakiwa katika afisi za Shirika la utangazaji la Royal Media Services mwezi Disemba 2019Akiiondoa kesi hiyo, Wanja aliiarifu mahakama kwamba alichukua uamuzi huo baada ya kumsamehe mwanasiasa huyoWanja ambaye huendesha mijadala katika runinga ya Inooro alikanusha madai kwamba alilipwa kuiondoa kesi hiyo mahakamanMahakana jijini Nairobi mnamo Alhamisi, Julai 22 ilimwachilia huru mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kuhusiana na kesi ambapo alimdhulumu mwanamke.

Hakimu Mwandamizi wa mahakama ya Milimani Martha Mutuku alimwachilia huru mwanasiasa huyo baada ya mlalamishi Wanja kuondoa kesi hiyo kortini.

"Nimemruhusu mlalamishi kuondoa kesi dhidi ya mtuhumiwa Mbunge Moses Kuria chini ya kifungu 204 cha Makosa ya Jinai ninaamuru pia arejeshewe pesa taslimu alizolipa mahakama," Mutuku alisema.

Akiiondoa kesi hiyo, Wanja aliiarifu mahakama kwamba alichukua uamuzi huo baada ya kumsamehe mwanasiasa huyo.

Wanja ambaye huendesha mijadala katika runinga ya Inooro alikanusha madai kwamba alilipwa kuiondoa kesi hiyo mahakamani.



Read also

Kaburi Huficha Mengi: Maswali Yaibuka Kuhusu Kifo cha Caroline Kangogo

"Sikushurutishwa na mtu yeyote kwa njia yoyote ile au hata kushawishiwa na mtuhumiwa kuiondoa kesi mahakamani," aliiambia mahakama.

Kuria alikabiliwa na shutuma za kumshambulia Wanja katika afisi za shirika la Royal Media Services mwezi Disemba 2019.

Mbunge huyo alikuwa ameachiliwa kwa dhamana ya KSh 20,000.

Mapema mwaka huu mbunge huyo aliomba mahakama kumruhusu kutatua kesi hiyo nje ya korti.

Mbele ya hakimu Martha Mutuku mnamo Ijumaa, Januari 22, Kuria kupitia kwa wakili wake Goeffrey Omenkeh alisema anajadaliana na malalamishi ili watatue suala hilo nje ya korti.

Mbunge huyo alisema mlalamishi pia aliashiria kukubaliana naye.

"Tunajadiliana na mlalamishi ili kesi hiiitatuliwe nje ya mahakama. Pindi tu tutakapoafikiana tutaiondoa mahakamani," Omenke alisema.

Hakimu Mutuku alikuwa ameagiza kesi hiyo itajwe Februari 4, 2021 kuthibitisha iwapo pande zote mbili zilikuwa zimeafikiana kuhusu kutatua kesi hiyo nje ya mahakama.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.



Read also

Cate Waruguru Aashiria Kuhama Jubilee, Asema Haina Maisha

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke