Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye silaha nchini DR Congo kuweka chini silaha zao na kufanya kazi na Rais Félix Tshisekedi katika kuimarisha amani na utulivu katika nchi hiyo changa zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kenyatta alisisitiza kuwa bila kufanyia kazi umoja na utangamano miongoni mwa watu wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kila sehemu tofauti itasalia kuwa hasara. "...bila kuweka silaha chini na kuunda mkataba wa kitaifa usioweza kuvunjika ili kupatia DRC, matunda ya ustawi, ambayo ninyi nyote mnastahili yatabaki kuwa magumu.
"Hii inafanya kuwa muhimu kwa watu wote wenye nia njema nchini DRC kuungana pamoja na kuweka msingi wa ustawi kwa kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kuleta amani ya kudumu," Rais aliwaambia watu wa DR Congo.
Ujumbe wa Rais Kenyatta uliwasilishwa katika taarifa ya video iliyorekodiwa iliyotolewa Jumatano jioni wakati wa mazungumzo ya mtandaoni ya amani kati ya Congo yaliyoitishwa na Kenya.