Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta atoa wiki mbili ufumbuzi mahindi yaliyozuiliwa

Kenyatta Ed Kenyatta atoa wiki mbili ufumbuzi mahindi yaliyozuiliwa

Wed, 5 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kenyatta ametoa agizo hilo leo Mei 5, 2021 nchini Kenya katika kongamano la wafanyabiashara mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wiki chache zilizopita mahindi ya Tanzania yalizuiwa kuingia Kenya ikidaiwa kuwa na sumu kuvu jambo ambalo lililosababisha malori kukwama mpakani huku wafanyabiashara wakihangaika kutafuta  maeneo mengine ya kuuza bidhaa hiyo.

Wakati akilihutubia kongamano hilo, Kenyatta amesema Kenya na Tanzania ni nchi jirani na ndugu, hivyo hakuna sababu ya kuwekeana vikwazo vitakavyoumiza wananchi.

“Natoa maelekezo hapa, kwanza yale mahindi yaliyolala mpakani waziri nakupa wiki mbili hilo suala liwe limeisha. Pili mawaziri wanaohusika nendeni kutatua foleni iliyopo Taveta na Holili, kama suala ni vyeti vya Covid 19 hakuna haja ya mtu wa mataifa haya kupimwa mara mbili kama amechekiwa Tanzania basi aingie Kenya”

“Wawekezaji wa Tanzania mjue ya kwamba mna uhuru wa kuleta na kufanya biashara zenu hapa bila kuitishwa visa za biashara wala vibali vya kazi. Muwe huru kama mnavyokuwa Tanzania muhimu mfuate sheria na kanuni zilizowekwa.” amesema Rais Kenyata

Chanzo: ippmedia.com