Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta atangaza siku 7 za maombolezo

617858f4e09914f7581bc2d3dcc6c689 Kenyatta atangaza siku 7 za maombolezo

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KUFUATIA kifo cha Rais Magufuli, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa nchini humo ikiwa ni heshima ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyefariki jana usiku kwa ugonjwa wa moyo.

Rais Kenyatta ameagiza bendera ya Kenya na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ipeperushe nusu mlingoti kuanzia leo Machi 18 hadi Rais Magufuli atakapozikwa.

Katika hotuba iliyotolewa na Kenyatta mapema leo alimtaja Magufuli kama kiongozi mashuhuri na bingwa wa ukabila wa Kiafrika na kuongeza kuwa kwa upande wake amepoteza rafiki wa kweli.

"Kwa niaba ya Serikali na watu wa Kenya, ninawasilisha salamu za pole za dhati kwa Mke wa Rais wa Tanzania, Janeth Magufuli, watoto wao, familia nzima ya Magufuli na kwa kweli tunathibitisha mshikamano wetu wa kina na serikali na watu wa Tanzania wakati huu wa changamoto. Tanzania inabaki katika mawazo na maombi yetu, ”alisema Kenyatta.

Kifo cha Dk Magufuli kilitangazwa jana usiku na Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu ambapo alisema Magufuli amefariki kutokana na ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Jimbo la Mzena jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 61.

Chanzo: www.habarileo.co.tz