Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta alikua upinzani, Ruto abainisha

William Ruto 2 1140x640.jpeg Kenyatta alikua upinzani, Ruto abainisha

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: Dar24

Rais William Ruto wa Kenya amemtaja rais mstaafu wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kuwa alikua kiongozi wa chama cha Upinzani

William Ruto amebainisha hayo katika hotuba yake ya kwanza kwenye kikao cha pamoja cha Bunge wakati akihutubia kwa mara ya kwanza Alhamisi, Septemba 29, tangu kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo na pia akishuhudia kuapishwa kwa wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti.

Katika hotuba yake, Ruto aliwachekesha wabunge hao baada ya kusema kwa mzaha jinsi yeye, aliyekuwa naibu wa rais wakati huo, alivyokuwa mgombea wa urais kwa Upinzani huku kinara wa Upinzani, Raila Odinga, akiwa mgombeaji aliyefadhiliwa na serikali katika uchaguzi wa Agosti.

“D.P wa wakati huo akawa mgombea wa upinzani na kiongozi wa upinzani akawa mgombea wa serikali… mgombea wa upinzani alishinda uchaguzi na kuwa Rais na Rais akawa kiongozi wa upinzani. Huo ndio utamu wa demokrasia yetu,” alisema Ruto.

Chanzo: Dar24