Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta: Ruto ameshindwa kutimiza matakwa ya Wakenya

Kenyatta Pic Jino Kwa Jinooo Kenyatta: Ruto ameshindwa kutimiza matakwa ya Wakenya

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais mstaafu wa Kkenya, Uhuru Kenyatta, ameikashifu serikali ya Kenya Kwanza, kwamba “iimeshindwa kutimiza matakwa ya Wakenya”.

Akizungumza jana Jumapili, katika Kaunti ya Kitui, Bw Kenyatta alisema Rais William Ruto amefeli kutimiza ahadi zake kwa Wakenya.

Rais huyo mstaafu wa Kenya amesema Rais Ruto amekuwa akitoa visingizio vya mara kwa mara, Dkt anapotakiwa kueleza sababu za maisha kuzidi kulemea wananchi.

Bwana Kenyatta amesema serikali ya Kenya Kwanza imefanya vibaya sana, jambo ambalo ni kinyume na ahadi zake wakati Ruto na wenzake walipokuwa wakisaka kura 2022 kumrithi kuingia Ikulu.

Rais huyo mstaafu wa kenya amewachekeksha hadhirina kwa kusema: “Siku hizi ninalaumiwa kwa kila kitu na wale walio madarakani. Hata mke wa mtu akikosa kushika mimba, wanalaumu mimi Uhuru."

Wakati wa wa kampeni za uchaguzi wa rais 2022, Dkt William Ruto aliahidi kwamba akiapishwa rasmi, gharama ya maisha itashuka mara dufu, ikiwemo bei ya unga aliodai pakiti ya kilo mbili ya bidhaa hiyo ingeuzwa chini ya Sh100.

Hata hivyo Kinyume na ahadi zake, amepandisha ushuru (VAT) wa mafuta ya petroli na kuanzisha kodi zaidi, hatua ambayo imechochea gharama ya maisha ya Wakenya kupanda mara dufu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live