Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta: Rais Samia, tutashirikiana

7188e8bf60b712cd881b765f55818460.jpeg Kenyatta: Rais Samia, tutashirikiana

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyata amemtaka Rais wa sita, awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwa na moyo mkuu, asiogope kuichukua nchi katika kipindi kichungu cha majonzi.

Rais Kenyata ameyasema hayo akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Hayati Rais John Magufuli aliyefariki dunia, Machi 17 katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Nikupe neno moja dada yangu Samia, umeshika nchi kipindi kichungu cha majonzi, hata Joshua alipoachwa na Musa alijiuliza nitaweza kweli, lakini Mungu alimwambia usiogope, kuwa na moyo mkuu, nawe usiogope mungu yu pamoja nawe.” alisema na kuongeza

“Dada yangu Samia, kuwa na moyo mkuu usiogope, Mungu yu pamoja nawe kila uendapo, watanzania wapo nyuma yako.” alisisitiza Kenyatta.

Akimzunguzia hayati Rais Magufuli, Kenyatta alisema “Sote tunaomboleza kumpoteza rafiki yetu, mchapa kazi, Rais aliyeheshimika sio tu Tanzania hata Afrika Mashariki yote na dunia kwa ujumla.

“Muda wa miaka michache aliyokaa madarakani ameonyesha waafrika tunauwezo wa kujitoa kwenye utegemezi, kama Afrika tunauwezo wa kujitegemea wenyewe na kuzisimamia rasilimali zetu wenyewe.

Rais Kenyata alisema kwa muda mfupi pia wa hayati Magufuli wameshuhudia kazi kubwa aliyofanya ya ujenzi wa barabara, umeme, bandari na viwanja vya ndege ambavyo kama Jumuiya ya Afrika Mashariki watatumia kwa ajili kukuza biashara na kukuza uchumi.

Alisema “Dk Magufuli ni rafiki yangu tulikuwa tunaongea mara kwa mara kuhusu nchi zetu, kwangu binafsi kifo chake ni pigo kubwa, alikuwa ni mtu muhimu sana kwangu, nikasema liwalo na liwe lazima nije kumsindikiza ndugu yetu, tutaendelea kufanya kazi pamoja na watanzania na kuendeleza umoja wa Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz