Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta, Ndayishimiye watia  saini kuimarisha ushirikiano

5d817376142ef910fb493870406f73ad.jpeg Kenyatta, Ndayishimiye watia  saini kuimarisha ushirikiano

Tue, 8 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI za Kenya na Burundi zimetiliana saini makubaliano ambayo yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo.

Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Burundi Evariste Ndayishimiye walitia saini makubaliano katika ziara yake ya siku mbili ya kiongozi huyo wa Burundi.

Mikataba ya ushirikiano iliyotiwa saini ni ya ushirikiano wa kilimo, utumishi wa umma, masuala ya mambo ya nje ,biashara, michezo na utamaduni.

Akizungumza na waandishi wa habari,Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema nchi hizo mbili zimekubali kuimarisha uhusiano wao wa muda mrefu kwa lengo la kukuza maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

“Ushirikiano kati ya nchi zetu mbili umejengwa katika msingi thabiti wa maadili na kanuni za pamoja, kukuza maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi na mabadiliko ya nchi zetu mbili, Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nguvu na umoja, na Afrika iliyojumuishwa na yenye mafanikio, ”Uhuru alisema.

Aliongeza kuwa kuna fursa nyingi za kibiashara ambazo hazijatumika kati ya nchi hizo mbili na kuagiza wizara husika kupitia na kushughulikia vizuizi vinavyozuia ukuaji wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo.

Uhuru pia alitangaza azimio la Kenya na Burundi la kutanguliza elimu katika mipango yao ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, na kwamba nchi hizo mbili zitaunga mkono kampeni ya nne ya Global Partnership Education (GPE) kupata angalau dola bilioni tano kwa uwekezaji katika elimu.

Kama sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na Burundi, viongozi wawili walikubaliana kufufua Tume ya Kudumu ya Pamoja ya mwaka 2018 kwa nia ya kuhakikisha utekelezaji wa haraka wa makubaliano yaliyokubaliwa.

"Tunafurahia uhusiano kati ya nchi zetu mbili katika uwekezaji na biashara. Nakumbuka jukumu ambazo Kenya ilifanya katika kulinda amani nchini Burundi na kuwezesha biashara kupitia bandari ya Mombasa, na wawekezaji wa Kenya ambao tayari wanafanya kazi nchini Burundi, ”Alisema Rais wa Burundi Evaristi Ndayishimiye

Chanzo: www.habarileo.co.tz