Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yazindua jukwaa la kwanza la huduma za mwisho wa maisha

Kenya Yazindua Jukwaa La Kwanza La Huduma Za Mwisho Wa Maisha Kenya yazindua jukwaa la kwanza la huduma za mwisho wa maisha

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Kenya, kupitia kampuni ya kiteknolojia ya SafiriSalama.com, imezindua jukwaa la kwanza la huduma za mwisho wa maisha.

Jukwaa hilo litakuwa linatoa arifa za kifo cha kidijitali, ukumbusho, na jinsi ya kuwapata watoa huduma za mazishi.

Waanzilishi wa kampuni hiyo waliamua kutumia jina la "Safiri Salama," ambayo hutafsiriwa "Nenda kwa Amani", ili kujitosa katika huduma hiyo ya kidijitali ambayo ni geni sio Kenya tu bali pia barani Afrika.

"Waafrika wana mwelekeo wa kuepuka mijadala kuhusu kifo au mipango ya mwisho wa maisha," anasema John Nyongesa, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji.

"Ukosefu huu wa maarifa hufanya wanaoomboleza kutumiwa vibaya, kwani watu hawana habari na wanaweza kuathiriwa wakati mpendwa anapoaga dunia.

Anaongeza kuwa huzuni na maamuzi ya haraka yanapounganishwa, familia zilizofiwa huwa katika hali mbaya au duni.

"Familia zinazoomboleza zinakabiliwa na ugumu wa kufanya utafiti unaofaa na mara nyingi "kununua kwa shinikizo" kwa sababu ya ukosefu wa bei zilizochapishwa katika tasnia ya mazishi." Anasema Nyongesa

Sekta ya mwisho wa maisha nchini Kenya imeshuhudia ukuaji mkubwa katika miaka ya hivi karibuni, inayokadiriwa kuwa na thamani ya $450 milioni (KShs 56 bilioni) kila mwaka.

Hata hivyo, tasnia haina mfumo unaoeleweka na unaofaa mtumiaji kwa familia zilizofiwa, na hivyo kusababisha masuala kama vile bei kutofautiana, viwango visivyoeleweka vya sekta, na ugumu wa kutofautisha kati ya washindani.

Chanzo: Bbc